Serikali kupambana na wachimba mchanga

Monday , 17th Jul , 2017

Serikali imeahidi kupambana na kwa kufanya msako wa usiku na mchana kuhakikisha watu wanaochimba na kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi wanachukuliwa  hatua kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina

Hayo yamesemwa leo mapema na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina ambapo amesitisha shughuli za uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo mbalimbali yasiyo rasmi jijini Dar es salaam ili kuweza kuondokana na tatizo la uchafuzi wa mazingira.

Wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju amesema kuwa kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na ili kubaini kama kuna uwezekano wakuchimba mchanga.

Aidha, amesema kuwa ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Halmashauri pamoja na NEMC

“Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufuata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”amesema Mpina

Recent Posts

Mh. Mavunde akikabidhi mabomba kwa wananchi.

Current Affairs
Mavunde ajikita kwa wapiga kura wake

Wanafunzi wa Jangwani Sec kwenye picha ya pamoja na watangazaji wa
EATV na EA radio wakionyesha zawadi za taulo za kike walizopokea kutoka watanzania kupitia kampeni ya 'Namthamini'

Current Affairs
Shule za Kisutu, Jangwani zapata neema

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama

Current Affairs
Waziri Mhagama awapa siku 30 Waajiri

Mkuu wa kitengo cha elimu kwa uma kikosi cha usalama barabarani Mrakibu msaidizi wa Polisi ASP Mossi Ndozero.

Current Affairs
Ukaguzi magari hauna kikomo