Ma-adimin wa 'Whatsapp group' waonywa.

Monday , 17th Jul , 2017

Viongozi wa makundi ya mitandao ya kijamii hasa hasa 'Whatsapp' nchini Kenya wameonywa kujiepusha na kutuma ujumbe zilizokuwa na chuki katika kipindi cha uchaguzi kinachoenda kuanza siku chache zijazo.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya, Francis Ole Kaparo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uchaguzi Mkuu nchini humo, Francis Ole Kaparo huku akisisitiza kuwa hawawezi kufunga ama kuzuia watu wasitumie mitandao ya kijamii ila wanawataka waitumie kwa uwazi na umakini.

"Waambieni wasimamizi wa makundi ya WhatsApp wanaoruhusu kutumwa kwa ujumbe zenye chuki katika kipindi hiki cha uchaguzi, tunakuja kwa ajili yao,'We will not shut down the internet during elections but it must be used responsibly, tell administrators of WhatsApp groups fanning hate speech, we are coming for them", amesema Kaparo.

Kwa upande mwingine, ni mara ya kwanza leo kwa wagombea wenza wa urais (Makamu wa Rais) nchini Kenya wanakutana ana kwa ana kwenye mdahalo wa kihistoria utakaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Catholic University of Eastern Africa (CUEA) mjini Nairobi.

Wagombea wenza hao ni  Eliud Kariara,  Emmanuel Nzai,  Kalonzo Musyoka,  Miriam Mutua, Moses Marango,Orina Momanyi, Titus Ng'etuny pamoja na William Ruto